Mafuriko ya mvua yaathiri baadhi ya maeneo ya Tabora.

Wakazi wa kata ya Mpera iliyopo katika manispaa ya Tabora wamekumbwa na mafuriko hali iliyosababisha maji kuzingira nyumba zao huku mali zao zikiteketea na kusombwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora.

Hii ndiyo hali halisi iliyopo hapa katika mtaa wa Muhalitan almaarufu Freemason kata ya Mpera manispaa ya Tabora, wakazi wa eneo hili wameingiwa na hofu kubwa baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji kuanzia usiku wa kuamkia leo.

Jeshi la zima moto na uokoaji lilifika eneo hili na kuanza walau kuwanusuru watu waliokuwa ndani ya nyumba hizi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa, naye amefika eneo hili kuzungumza na wananchi huku akisisitiza zaidi suala la usalama wao.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Frederick Sumaye ajiondoa Chadema.

Read Next

Wafanyabiashara ya madini kutoa taarifa kwa mtandao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram