Fursa ya masomo ya elimu ya juu nchini Ufaransa.

Serikali kupitia Wizara zinazosimamia masuala ya Elimu Tanzania Bara na Zanzibar kwa kushirikiana na Ubalozi wa Ufaransa hapa Nchini zimeandaa kongamano kubwa la vyuo vya elimu ya juu kati ya Ufaransa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Disemba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo ambalo litashirikisha vyuo vikuu kutoka Ufaransa na Tanzania ambavyo vitatoa taarifa muhimu za udahili na kozi zitolewazo lengo likiwa ni kusaidia juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuendeleza elimu ili kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi hususani Tanzania.

Akizungumzia Kongamano hilo litakalofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius nyerere jijini Dar es Salaam, Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Bw. Frederic Clavier amesema kufungua zaidi milango kwa Watanzania Kutumia fursa za ufadhili wa masomo ya ujuzi mbalimbali iliyotolewa na Serikali yake.

Kongamano hilo pia litafunguliwa na kuhudhuriwa na Prof. Joyce Ndalichako, Makampuni na wawekezaji kutoka Ufaransa, Wahitimu wa vyuo na taaluma mbalimbali za nchini Ufaransa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mhadhiri mwandamizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam ambacho ni Chuo mshirika wa Chuo kiku cha Bordeaux cha nchini Ufaransa, ameainisha baadhi ya fursa zitakazofunguliwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mvua zakata mawasiliano ya Simiyu, Shinyanga na Mara.

Read Next

Frederick Sumaye ajiondoa Chadema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram