Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa zimeleta adha kwa watumiaji wa Barabara inayounganisha Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mara na Nchi Jirani ya Kenya baada ya Daraja la Mto Simiyu linalounganisha maeneo hayo kufurika maji kwa zaidi saa nne huku mvua hizo zikiharibu Makazi ya watu, mali na Mashamba.
Badhi ya Wakazi ya Kata ya Zanzui Wilayani Maswa ambao nyumba zao ziliharibiwa vibaya na mvua hizo wanaeleza namna walivyojikuta wanapoteza mali na mazao yao waliyolima.
Lakini Licha ya Mvua hizo kuwa hatari kwa maisha ya watu wanaoishi karibu na maeneo ya Daraja hilo, baadhi yao wakazitumia kupata kitoweo cha samaki kwa kuanza kuvua samaki.
Hata hivyo daraja ambalo linajengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Chiko inayojenga barabara hiyo lililazimika kutumika kwa muda licha ya ujenzi wake kutokamilika.