Frederick Sumaye ajiondoa Chadema.

Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye amejitoa kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Sumaye amesema kitendo cha kutaka kuchukua fomu kutaka kugombea wenyekiti wa chama hicho taifa kimempelekea mwenyekiti Freeman Mbowe na kuwashinikiza wajumbe wa kanda kwamba wasimpigie kura.

Aidha amesema hakuhamia upinzani kwa chuki ya Ccm ambapo amesema kuwa vyama vya upinzani vinapaswa kuwa na demokrasia ya kweli kuanzia katika vyama hadi taifani.

Amesema kuwa aling’amua kuwa Kujiunga upinzani si kazi rahisi hasa kwake kwani uchaguzi wa kanda aliletewa fomu na kuijaza na kushangiliwa lakini baadae alikutana na misukosuko mikubwa na kuwa nongwa baada ya kuijaza fomu ya uwenyekiti wa chama hicho.

Sambamba na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kujiondoa uanachama Chadema bado anaamini kuwa Upinzani sio uadui ataendelea kutia ushauri kwenye vyama vingine vingi nchini.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Fursa ya masomo ya elimu ya juu nchini Ufaransa.

Read Next

Mafuriko ya mvua yaathiri baadhi ya maeneo ya Tabora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram