Maonyesho ya Utalii karibuni Kusini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amesema ameridhishwa na mafanikio yaliyofikiwa katika kuvitangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana kwenye mikoa ya Kusini Nyanda za Juu huku akitaka juhudi zaidi zielekezwe kwenye dhana ya uimarishwaji wa miundombinu kwenye vituvitio hivyo.

Akiongea kwenye ufunguzi wa kikao cha kufanya tathmini ya kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Utalii kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini (KARIBU KUSINI), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amesema maonyesho hayo kwa mwaka 2019 yalikuwa na mafanikio makubwa hasa ktk mkakati wa kutangaza maeneo yenye vivutio vya utalii kwa mikoa hiyo ambayo ina rasilimali kubwa zinazoweza kutumika kuliingizia Taifa mapato kwa kiasi kikubwa huku Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Tawala wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Happiness Seneda akitoa ushauri wa ushirikishwaji wa sekta binafsi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Uhuru Media Group (UMG) Josephat Mwanzi amevitaka vyombo vya habari nchini kuona fahari kuitangaza nchi kiutalii. Kikao hicho cha tathmini kimekutanisha makatibu tawala wa mikoa ya nyanda za juu kusini.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali Kahama yatambua maeneo ya uchimbaji Madini.

Read Next

Mvua zakata mawasiliano ya Simiyu, Shinyanga na Mara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram