TMDA yafanikiwa kudhibiti bidhaa mbovu.

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba – TMDA imesema katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2015 hadi 2019 wamefanikiwa kudhibiti bidhaa zinazoingia nchini ambapo hivi sasa Usalama wa Bidhaa katika soko Umeimarika na kufikia Asilimia 96.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dsm Kaimu Meneja Mkuu wa TMDA Adam Fimbo amesema katika Kipindi cha Miaka minne ya Mafanikio, Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba ambayo inajukumu la kudhibiti Ubora, Usalama na Ufanisi wa Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi ili kulinda afya ya Jamii imefanikiwa kudhibiti bidhaa zisizo na Ubora katika soko la Tanzania.

Aidha Bw. Fimbo amesema katika kipindi cha Mwaka 2017/18 kiasi cha Tani 140,705 za Bidhaa za chakula, dawa na Vifaa tiba zisizofaa kwa matumizi ya Binadamu zenye Thamani ya Shilingi bilioni 22 ziliteketezwa ikilinganishwa na Tani 664,68 zilizoteketezwa mwaka 2018/19 na kuashiria kupungua kwa bidhaa zisizokidhi viwango katika Soko la Tanzania.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Kupanda Mlima Kilimanjaro.

Read Next

Watu kadhaa wamenasa katika kifusi baada ya jengo la ghorofa sita kuanguka Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram