Watu kadhaa wamenasa katika kifusi baada ya jengo la ghorofa sita kuanguka Kenya.

Vikosi vya usalama nchini Kenya vimeripoti kuwa watu kadhaa huenda bado wamenasa katika kifusi baada ya jengo la ghorofa sita kuanguka asubuhi ya leo katika eneo la Embakasi jijini Nairobi.

Shughuli za uokoaji zinaendelea huku ripoti zikisema watu kadhaa wameokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Watu watatu wakiwa na majeraha mabaya wametolewa kutoka kwenye kifusi na kupelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya Kenyatta, jijini Nairobi, wakiwemo mama na mtoto.

Inaelezwa kwamba zaidi ya familia 46 walikuwa wakuwa wakiishi kwenye jengo hilo ambalo limeanguka asubuhi ya kuamkia leo.

Polisi na kikosi cha msalaba mwekundu kutoka kaunti ya Nairobi wako kwenye eneo la tukio ingawa vikosi hivyo pia vinakabiliana na wakati mgumu kutokana na msongamano wa kudhibiti kundi kubwa la watu waliojitokeza kushuhudia mkasa huo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TMDA yafanikiwa kudhibiti bidhaa mbovu.

Read Next

Mafuriko wilayani Magu Kaya zimezingirwa na maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram