CECAFA: Zanzibar Heroes yalala 1-0 dhidi ya Kili Stars.

Tanzania Bara imefufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zanzibar katika Uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda.

Pongezi kwa mfungaji wa bao pekee la Kilimanjaro Stars, mshambuliaji wa Azam FC, Ditram Nchimbi Duma anayecheza kwa mkopo timu ya Polisi Tanzania, zote za Ligi Kuu ya Bara.

Nchimbi, mchezaji wa zamani wa Njombe Mji FC, Maji Maji ya Songea na Mwadui FC, alifunga bao hilo dakika ya 39 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Suleiman Ahmed Ali Selula kufuata shuti la mshambuliaji wa Buildcon ya Zambia, Eliuter Mpepo aliyemalizia pasi ya kiungo wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude.

Katika mechi nyingine ya kundi hilo, Uganda iliibuka na ushindi wa magoli 2-1 kwa sifuri dhidi ya Sudan.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Wanachama wa Chadema wahamia CCM.

Read Next

Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!