Matembezi maalumu ya kukusanya fedha.

Waziri wa Utalii na Maliasili Dkt.Khamis Kigwangala ameongoza matembezi maalumu ya kukusanya fedha kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu na yatima wapatao 80 wa kituo cha VID Upanga jijini Dar es salaam.

Mara baada ya matembezi hayo ulifanyika mnada maalum wa kuchangia fedha ambazo zitawezesha wanafunzi kupata mahitaji yao maalum yakiwemo ya shule kwani idadi iliyopo katika kituo hicho ni kubwa.

Akizungumza katika hafla hiyo mwanachama wa kituo hicho cha VID Neyma Besta amesema Waziri Kigwangala amewaunga mkono kwa kiasi kikubwa ikiwepo kuwahamaisha wananchi kujitokeza kuwasaidia watoto yatima ili waweze kupata amahitaji yao.

Bi. Neyma amesema fedha zote ambazo zimepatikana zitaelekezwa katika mahitaji maalumu ya watoto hao ambao katika kituo hicho ni wengi na wanahitaji msaada mkubwa ambapo ametoa wito kwa taasisi na makampuni kujitolea kusaidia watoto wa kituo hicho.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Maandamano nchini India.

Read Next

Wanachama wa Chadema wahamia CCM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!