Wanachama wa Chadema wahamia CCM.

Katibu wa Wilaya wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Wilayani Mbogwe, mkoani Geita, Kazimiri Maduka amekihama rasmi chama hicho pamoja na wanachama wenzake 25 na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti wa CCM Wilayani Mbogwe, Johari Juma amewapokea wanachama hao wa CHADEMA katika hafla fupi iliyofanyika katika kijiji cha Busulilo kata ya Iponya na kutoa wito kwa wana CCM kuwapa ushirikiano kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM Kiongozi huyo wa zamani wa upinzani na mwenyekiti wa serikali ya kijiji iliyopita amesema, kujitoa CHADEMA kushiriki uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka huu kulimvunja moyo kuendelea na harakati za kuongoza Chama hicho.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Matembezi maalumu ya kukusanya fedha.

Read Next

CECAFA: Zanzibar Heroes yalala 1-0 dhidi ya Kili Stars.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!