Wazazi wahimizwa kuwaandaa watoto kimaadili.

Katika kuliandaa Taifa lenye maadili mema na uwajibikaji taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Manyara imetembelea wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Babati Mrara jana ikiwa ni siku ambayo Tanzania huadhimisha siku ya maadili ambapo wazazi wametakiwa kuwandaa watoto kwenye misingi ya maadili bora na wenye uzalendo.

Asili ya siku ya maadili kitaifa inatokana na mapatano ya umoja wa mataifa yaliyofanyika 2003 katika mji wa Merida. Mapatano hayo yalilenga mapambano dhidi ya rushwa ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika mataifa mengi duniani ikiwa zaidi nchi za bara la Afrika.

Katika mkoa wa Manyara taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa imetembelea Hospitali ya Mrara katika wodi hii ya wazazi ikiwa mama ni msingi mkubwa wa familia.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho haya mwaka 2019 ni ‘maadili katika Utumishi wa Umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu’.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Shirika la Posta laanda shindano.

Read Next

Aliyetoka kwa msamaha wa Rais akamatwa kwa kutaka kuiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!