Maazimio ya Mkutano Mkuu wa NEC.

Chama cha mapinduzi kimetoa taarifa kwa umma kuhusu maazimo ya mkutano wa Halamashauri kuu ya chama hicho NEC uliofanyika jijini Mwanza.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu wa NEC – Itikadi na Uenezi wa chama hicho ndugu Humphrey Pole Pole inasomeka kama ifuatavyo:

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeketi leo Jijini Mwanza chini ya Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) ni wa kawaida kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kabla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa wajumbe walifanya ziara ya kukagua miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza. Wajumbe pia walipata muda wa kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha Miaka Minne ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Maandalizi na maudhui ya Mwelekeo wa Sera za CCM kwa Mwaka 2020 ñ 2030 sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (HKT) wameazimia kwa kauli moja kupongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Ndugu Rais John Pombe Joseph Magufuli na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayo ongozwa na Ndugu Rais Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambapo mafanikio makubwa ya kimaendeleo yamepatikana.

Halmashauri Kuu ya Taifa imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.

Wanachama hao ni;-

  1. Ndg. Januari Makamba (Mb)
  2. Ndg. Nape Nnauye (Mb) na,
  3. Ndg. William Ngeleja (Mb)

Kikao cha HKT kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama.

Wakati Huo huo, Halmashauri Kuu ya Taifa (HKT) imeazimia kwa kauli moja na kuelekeza kwamba wanachama wafuatao;-

1 Abdulrahman Kinana
2.Mzee Yusuf Makamba na,
3.Benard Membe

Waitwe na Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli aongoza kikao cha NEC.

Read Next

BOT yatakiwa kudhibiti utapeli sekta ya huduma ndogo za fedha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!