Rais Dkt. Magufuli aongoza kikao cha NEC.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi na kuwapongeza wajumbe wa kikao hicho kwa kuiongoza vyema Serikali.

Mhe. Rais. Dkt. John Pombe Magufuli amewaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa mafanikio yote yaliyopatikana katika miradi mikubwa inayondeshwa na Serikali ya awamu ya tano ni utekelezaji wa maazimio yaliyotolewa na wajumbe wa mkutano huo kwa Serikali.

Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa Semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama cha Mapinduzi jana, Mhe. Rais. Dkt. John Pombe Magufuli alizungumzia kwa kina miradi yote mikubwa inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano.

Nao wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi walionyesha imani kubwa ya utekekelezaji wa Ilani ya chama hicho katiak ngazi ya taifa kama inavyofanywa na Rais. Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Waziri Mbarawa amuweka ndani mkandarasi.

Read Next

Maazimio ya Mkutano Mkuu wa NEC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!