Hatimaye Bombardier Q 400 yawasili nchini.

Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amewaongoza Watanzania jijini Mwanza kuipokea ndege aina ya Bombardier Q 400 iliyokuwa ikishikiliwa nchini Canada.

Ndege hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu,iliwasili jana katika uwanja wa ndege wa Mwanza huku viongozi mbalimbali wa ngazi ya taifa wakishuhudia.

Akizungumza awali kabla ya kuwasili kwa ndege hiyo,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amesema Serikali imejipanga kuimarisha usafiri wa anga nchini, ambapo imechukua hatua kadhaa ikiwemo kununua ndege mpya ili kuhakikisha kwamba usafiri huo unaimarika.

Aidha, Mhe.Rais,Dkt.John Pombe Magufuli amelipongeza Shirika la Ndege Tanzania na watendaji wote kwa kufanya kazi nzuri ya kuhakikisha usafiri wa anga unaimarika nchini.

Makubaliano ya kuikabidhi ndege hiyo ya Serikali aina ya Bombardier Q 400 kwa Shirika ya Ndege la Tanzania (ATCL) yamefanyika katika uwanja wa ndege wa Mwanza kabla ya ndege hiyo kuwasili.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

RC Arusha ataka kila Kaya Longido kufuga Mifugo.

Read Next

TRC na mfumo wa kupokea maoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!