RC Arusha ataka kila Kaya Longido kufuga Mifugo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewaagiza viongozi wote wa wilaya ya Longido kuweka mikakati katika kuhakikisha kila Kaya inafuga mifugo ya kutosha ili kuweza kukidhi mahitaji ya kiwanda cha kuchakata nyama kilichopo wilayani humo.

Gambo ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye uzinduzi na uwezeshwaji wa vikundi vya Wafanyabiashara wa mifugo na vya ushirika soko la kimataifa la mifugo Eworendeke wilayani Longido .

Amesema kuwa,kutokana na mahitaji makubwa ya mifugo yaliyopo kwa siku katika kiwanda hicho kuna haja kubwa kwa wananchi hao kuhakikisha wanakuwa na mifugo ya kutosha ili iweze kukidhi mahitaji yaliyopo ya ng’ombe,mbuzi na kondoo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido, Juma Mhina amesema kuwa, kutokana na uwepo wa kiwanda hicho wameona kuna haja ya kuvishirikisha vikundi mbalimbali na kuweza kupata fursa ambapo amesema ,hadi sasa zaidi ya vikundi Mia moja vimeshasajiliwa huku vikundi vya Wafanyabiashara 30 vikiwa vimesajiliwa pia, na kuongeza kuwa wilaya hiyo ina makisio ya ng’ombe 217,000,mbuzi 344,000,na kondoo 301,000.

Mkuu wa wilaya ya Monduli ,Frank Mwaisumbe amesema kuwa, uwepo wa kiwanda hicho umeweza kupunguza changamoto kubwa iliyokuwepo ya kutumia gharama kubwa kupeleka mifugo nchini Kenya kwani kwa Sasa hivi Wakenya wananunua mifugo hapa nchini.

Kwa mijibu wa mkuu wa wilaya hiyo kiwanda hicho kitakuwa kinapokea mbuzi na kondoo elfu nne kwa siku na ng’ombe Mia tano kwa siku.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Wakazi wa Ukarawa Lupembe walia na Uhaba wa Maji.

Read Next

Hatimaye Bombardier Q 400 yawasili nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!