Wakazi wa Ukarawa Lupembe walia na Uhaba wa Maji.

Wakazi wa vijiji vya Ukarawa na Kitole, Tarafa ya Lupembe wilayani Njombe wamemuomba Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa kuharakisha kukamilisha ukarabati wa mradi wa maji wa vijiji ambao umekwama kukamilika kwa kipindi cha miaka sita ili kuwaondolea adha ya muda mrefu ya kupanda na kushuka milima kufuata maji safi na salama mabondeni.

Atu Nduye mkazi wa kata ya Ukarawa Tarafa ya Lupembe mkoani Njombe akibainisha moja ya kero inayowapata kuhusu changamoto ya maji mbele ya Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa alipozungumza na wakazi wa kata hiyo juu ya serikali ilivyokusudia kutatua kero wanayoipata.

Mradi wa maji wa Ukarawa Wilayani Njombe ulioanza kujengwa mwaka 2013 kwa mkandarasi kupewa zaidi ya shilingi milioni 300 na haukukamilika kwa wakati na baadae serikali kutoa zaidi ya shilingi milioni 180 kwa ajili ya ukarabati wa mradi huo, ambapo Mbunge wa Jimbo la Lupembe, Joram Hongoli anasema takribani vijiji 12 havina maji safi na salama.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Ufaransa yaridhia ombi la Tanzania kufundisha Kiswahili.

Read Next

RC Arusha ataka kila Kaya Longido kufuga Mifugo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!