Jkt kuanza na wenyeji leo, Klabu Bingwa kikapu Afrika – Rwanda.

Wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya klabu bingwa barani Afrika ya Mchezo wa Mpira wa Kikapu Jkt, leo watashuka dimbani kucheza mechi yao ya kwanza ya michuano ya raundi ya pili ya kufuzu dhidi ya timu ya Patriots ambao ndiyo mabingwa wa Rwanda.

Mechi hiyo ambayo inapigwa kwenye uwanja wa Kigali Arena nchini Rwanda inatarajiwa kuchezwa majira ya saa mbili usiku kwa majira ya Afrika Mashariki.

Baada ya mechi yao ya leo dhidi Patriots katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufikia tamati Disemba 22, Jkt watacheza mechi nyingine kesho saa tisa alasiri dhidi ya Gendarmerie ya Madagascar.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Athari za mvua jijini Dar es Salaam.

Read Next

Rais Magufuli mgeni rasmi ufunguzi Mahakama Wilaya ya Chato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!