Vitisho vya mashambulizi ya kigaidi Kenya.

Jeshi la polisi nchini Kenya limetoa wito kwa wananchi kuwa makini kufuatia vitisho vya uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya kigaidi katika msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka za Christmas na mwaka mpya.

Akizungumza na televisheni binafsi K24 Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai amewataka wananchi kuwa waangalifu katika maeneo ya kuabudu pamoja na vituo vya usafiri wa umma.

Tahadhari hii imekuja baada ya polisi nchini humo kuwakamata washukiwa wa kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia baada ya kutekwa kwa wafanyakazi wanne wa kampuni ya ujenzi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Licha ya juhudi kubwa zilizopigwa katika kupambana na ugaidi nchini humo Jeshi la Polisi linasema bado kuna tishio na kila mmoja anapaswa kuwa makini wakati huu polisi wakiimarisha usalama katika maeneo ya umma nchini humo.

Kenya imeendelea kukabiliana na matishio ya ugaidi tangu mwaka 2011 baada ya kutuma jeshi lake nchini Somalia kupambana na kundi la Al Shabab.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Semina kuhusu ugonjwa wa Ebola.

Read Next

Maziwa ya mama ni kwa watoto tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram