Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya Posta duniani.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa maadhimisho ya miaka 40 ya Umoja wa Posta Afrika PAPU yatakayofanyika jijini Arusha januari 17-19 na kushirikisha washiriki zaidi ya mia tano (500) kutoka nchi 45 barani Afrika na wawakilishi wa umoja wa posta duniani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe amesema maadhimisho hayo ni ya kihistoria kwa nchi ya Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla na kuongeza kuwa maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa nchi wanachama kujitathmini katika eneo la utoaji wa huduma za Posta na kutoa fursa kwa nchi wanachama kubadilishana uzoefu juu ya hatua mbalimabli zilizofikiwa na nchi hizo katika kuboresha huduma za posta.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni ‘Posta mshirika wa uhakika katika kutoa huduma za fedha kwa wananchi wengi na kukuza ushirikiano wa kikanda‘ ambapo waziri huyo amesema kwa nchi ya Tanzania shirika la posta la Tanzania ni taasisi ya umma yenye mtandao mpana zaidi kwa kutoa huduma zake na uwakala kwa taasisi nyingine muhimu katika Nyanja ya uchumi na masuala ya kijamii.

Awali mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametoa wito kwa wafanyabiashara na wakazi wa jiji la Arusha na maeneo ya jirani kutumia mkutao huo kama fursa ya kujiongezea kipato katika kipindi ambacho wageni hao watakuwa nchini.

Katika kipindi cha maadhimisho hayo ya siku tatu kitaenda sambamba na maonesho ya sekta ya posta ambayo yatahusisha teknolojia, mitambo na vitendea kazi mbalimbali vya posta, pia katika maadhimisho hayo pia kutakuwa na hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya umoja wa posta Afrika ambalo limepangwa kujengwa jijini Arusha.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Takangumu zachangia kuziba mikondo ya maji.

Read Next

Wanawake wanaojiuza Manyara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram