Jenerali Gaid Salah wa Algeria afariki dunia.

Jenerali Ahmed Gaid Salah ambaye alikuwa mkuu wa majeshi nchini Algeria, alipata umaarufu mkubwa baada ya kumshinikiza rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika kujiuzulu.

Baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwezi Aprili, Jenerali Salah alichukua madaraka kwa muda katika kipindi cha mpito.

Jenerali Salah, mmoja wa wapiganaji wa zamani wa nchi hiyo wakati wa vita vya uhuru kati ya mwaka 1954 hadi 1962 dhidi ya Wafaransa amefariki dunia Jumatatu wiki hii baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Pamoja na kukumbukwa kumshinikiza rais wa zamani Bouteflika kuachia madaraka alishiriki kuandaa Uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi huu licha ya maandamano makubwa ya kupinga uchaguzi huo.

Serikali ya Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo na tayari Jenerali Said Chengriha ametangazwa kuwa mkuu mpya wa Majeshi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Kuanza matumizi ya tiketi za kielektroniki TRC.

Read Next

Wazazi washikiliwa kwa mauaji ya mtoto wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram