76 wafariki dunia katika mlipuko Mogadishu.

Bomu la kutegwa ndani ya gari limelipuka katika kituo kimoja cha ukaguzi wa usalama katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuuuwa takribani watu 76 na wengine sabini kujeruhiwa vibaya.

Msemaji wa serikali ya Somalia Ismail Mukhtar amesema idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu zaidi ya watu 70 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu.

Hili ni shambulizi baya zaidi kutokea katika siku za karibuni mjini Mogadishu huku mlipuko huo ukielezwa ulikilenga kituo cha kukusanya kodi wakati wa pilikapilika za asubuhi ambapo wakazi wakirejea kazini baada ya mapumziko ya mwishoni mwa juma.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mmoja Handeni anaswa wizi wa miundombinu.

Read Next

Mvua yaathiri makazi na miundombinu Dsm.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram