Mazishi ya Jenerali wa Iran, baadhi wamepoteza maisha.

Kituo cha televisheni cha serikali ya Iran kimeripoti kutokea kwa mkanyagano wakati wa mazishi ya jenerali Qassem Soleiman katika mji aliozaliwa, ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Mapema leo Wairani walianza kukusanyika kwa maelfu katika mji wa Kerman kwa ajili ya hatua za mwisho za mazishi ya Jenerali huyo aliyeuawa Ijumaa iliyopita katika shambulizi la Marekani nchini Iraq.

Picha za televisheni zimeonyesha idadi kubwa ya waombolezaji waliojitokeza katika miji ya Tehran, Qom, Mashhad na Ahvaz kwenye kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo wa kikosi maalum cha Quds – tawi la nje la jeshi la Iran.

Kuuawa kwa Jenerali Soleimani kumezua vita vya maneno kati ya Iran na Marekani, kila upande ukiapa kuchukua hatua za kulipiza kisasi.

Akizungumza mbele ya kundi la waombolezaji katika mji wa Kerman alikozaliwa Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa jeshi la mapinduzi la Iran, Hossein Salami, ametishia kuteketeza maeneo yanayopata msaada kutoka Marekani kufuatia kuuawa kwa Jenerali Soleiman.

Kauli yake inaakisi matakwa ya viongozi na maafisa wa ngazi ya juu wa Iran akiwemo kiongozi mkuu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei kutaka kulipiza kisasi dhidi ya Marekani kutokana na mauaji hayo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TMA yatoa taarifa kuhusu ongezeko la hali ya joto.

Read Next

Miradi inayotekelezwa yaboresha mandhari ya jiji Dsm.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!