Iran yaapa kuendeleza mashambulizi dhidi ya Marekani.

Kiongozi Mkuu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema kwamba mashambulizi ya makombora yalilofanywa na Iran kwenye kambi za kijeshi zinazotumiwa na Marekani nchini Iraq ni kofi la uso kwa Marekani ingawa amesisitiza hatua hiyo ya kijeshi bado haitoshi.

Akihutubia taifa lake baada ya Iran kufanya mashambulizi hayo, Ayatollah Khamenei amesema mashambulizi hayo ni yakulipa kisasi dhidi ya mauaji ya Jenerali wa kikosi maalumu cha Quds cha Iran, Qassemi Soleiman aliyeuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani mjini Baghdad Ijumaa iliyopita.

Amesema uwepo usio halali wa Marekani kwenye ukanda huo unatakiwa kukomeshwa kwani amesema umesababisha vita, mgawanyiko na uharibifu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohamad Zarif amesema mashambulizi hayo ni sawa na hatua za kujilinda huku Rais wa halmashauri ya Ulaya Ursula von der Leyen akitoa mwito wa kutafuta suluhisho la kidiplomasia la mvutano uliopo. Rais Donald Trump alitarajiwa kutoa tamko mapema kesho asubuhi kwa saa za Marekani.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa jijini Dsm.

Read Next

Mmiliki wa dampo lisilo rasmi akamatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!