Iran yashambulia ngome za Jeshi za Marekani.

Wizara ya ulinzi ya Marekani imethibitisha kuwa Iran imezishambulia kwa makombora kambi zake mbili zilizoko Iraq ambazo zinawahifadhi wanajeshi wa Marekani na majeshi ya muungano yaliyoko nchini humo.

Msemaji wa wizara hiyo, Jonathan Hoffman amesema ni wazi kwamba makombora hayo yamerushwa kutoka Iran. Hoffman amesema kambi za kijeshi zilizoshambuliwa ziko Ain Assad na Erbil.

Televisheni ya taifa ya Iran imesema shambulizi hilo ni katika kulipa kisasi mauaji ya jenerali wa ngazi ya juu wa nchi hiyo, Qassem Soleimani aliyeuawa na Marekani.

Hoffman amesema kambi hizo zimekuwa katika tahadhari ya juu kutokana na kuwepo dalili kwamba utawala wa Iran unapanga kuwashambulia wanajeshi wa Marekani na maslahi ya nchi hiyo katika eneo la Mashariki ya Kati.

Amesema Marekani itahakikisha inachukua hatua zote muhimu kuwalinda na kuwatetea raia na wafanyakazi wake pamoja na washirika wao katika ukanda huo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wanahabari wakumbushwa elimu kuelekea 2021.

Read Next

Wizi wa vifaa vya umeme Ruvuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!