Iran yagoma kutoa kisanduku cha ndege ya Ukraine.

Iran imesema haitakabidhi kisanduku cha kunakili safari ya ndege ama ”Black box” ya ndege ya Ukraine iliyopata ajali na kuua watu 176, kwa kiwanda kilichotengeneza ndege hiyo au kwa Marekani.

Ndege hiyo ya Ukraine aina ya Boeing 737-800 ilianguka muda mfupi baada ya kuanza safari yake kutokea uwanja wa ndege wa Tehran na hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo.

Kiongozi wa shirika la anga la Iran Ali Abedzadeh alinukuliwa katika vyombo vya habari nchini humo akisema hawatatoa kisanduku cheusi kwa Kampuni iliyotengeneza ndege hiyo na kuongeza kuwa tukio hilo litachunguzwa na Shirika la anga la Iran lakini Ukraine itaruhusiwa kuwepo wakati uchunguzi ukiendelea.

Ajali hiyo imetokea wakati ambapo kuna mvutano mkubwa kati ya Marekani na Iran, muda mfupi baada ya Iran kushambulia kwa makombora kambi mbili za kijeshi za Marekani zilizopo Iraq japo hakuna ushahidi kuwa matukio hayo mawaili yanahusiana na kuanguka kwa ndege hiyo

Shirika la Boeing lilisema kuwa liko tayari kusaidia kwa namna yeyote itakayohitajika, wakati huohuo waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau alisema alitarajia nchi yake ina wajibu wa kufanya uchunguzi kuhusu ajali hiyo na iko tayari kutoa msaada wowote wa kiufundi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wazazi wasiowapeleka shule watoto kuchukuliwa hatua.

Read Next

Waziri aagiza waliogoma kukaguliwa SACCOS wakamatwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!