Marekani yaelezea utayari kufanya mazungumzo na Iran.

Marekani imesema iko tayari kujadiliana na Iran bila masharti kuondoa uhasama uliozuka baina ya nchi hizo kufuatia mauaji ya Jenerali wa Iran Qasim Soleimani.

Katika waraka wake kwa Umoja wa Mataifa, Marekani imejitetea kuwa imemuua Jenerali wa Jeshi la Iran Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda. Iran kwa upande wake nayo ilizishambulia kwa makombora kambi za Majeshi ya Marekani nchini Iraq japo hakuna mtu aliyejeruhiwa au kuuawa.

Jenerali Soleimani alikuwa afisa wa pili wa ngazi ya juu nchini Iran kama Mkuu wa Kikosi Maalum cha Quds Force, katika Jeshi la Ulinzi la Revolutionary Guards’ na alikuwa mtekelezaji wa sera za Iran katika eneo la Mashariki ya Kati.

Katika hatua nyingine Baraza la wawakilishi la Bunge la Marekani lilitarajiwa kupiga kura leo ya kudhibiti uwezo wa Rais Donald Trump kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Iran wakati shutuma za Democrats dhidi ya mashambulizi ya Marekani yaliyomuua jenerali wa ngazi ya juu ya Iran zikiendelea.

Spika wa Baraza hilo Nancy Pelosi, alitangaza kura hiyo katika taarifa ambayo inasema shambulio la wiki iliyopita la ndege isiyo na rubani ambalo lilimuuwa Jenerali Soleimani ni uchokozi na limevuka mipaka. Azimio la Chama cha Democratic la madaraka ya vita linaonekana litapitishwa licha ya upinzani mkali wa chama cha Republicans.

Kutokana na mzozo wa kiutendaji baina ya vyama hivyo viwili, haifahamiki iwapo kura hiyo ya leo itakuwa hatua ya dhati kuelekea kumdhibiti Rais Trump kuhusu Iran ama itakuwa ni ishara tu ya upinzani wa chama cha Democrats.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Ripoti ya awali Iran kuhusu ndege iliyoanguka yatolewa.

Read Next

Dkt. Shein azindua daraja la Kibonde Mzungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!