Ripoti ya awali Iran kuhusu ndege iliyoanguka yatolewa.

Ripoti ya awali ya Iran iliyotolewa leo kuhusiana na ajali ya Ndege ya Ukraine iliyoanguka nchini humo jana imeeleza kuwa Rubani wa ndege hiyo hakutoa taarifa yeyote ya kuomba msaada na alikuwa akijaribu kurejea katika uwanja wa ndege kabla ya ndege hiyo kuanguka na kuua watu wote 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa hali ya dharura ilitokea kwenye ndege hiyo Boeing 737 ya shirika la ndege la Ukraine mapema siku ya Jumatano asubuhi, wakati ilipoanguka muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Wakati huo huo Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amesema wachunguzi wa ajali hiyo kutoka nchini mwake wamewasili nchini Iran kusaidia katika uchunguzi huo. Aidha Rais huyo alitarajia kuwasiliana na njia ya simu na Rais Hassan Rouhani wa Iran kuzungumzia kuhusu ajali hiyo pamoja na uchunguzi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mtu mmoja akutwa amefariki msituni Handeni.

Read Next

Marekani yaelezea utayari kufanya mazungumzo na Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!