Kiwanda chafungiwa kwa kukiuka kanuni na sheria za mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene amekifungia kiwanda cha kuzalisha nondo cha Fujian Hexingwang kilichopo Kisemvule Mkoa wa Pwani kwa kusababisha uchafuzi wa mazingira katika makazi ya watu na kukiuka sheria na kanuni za mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kiwandani hapo, Waziri Simbachawene amewataka wamiliki wa kiwanda kukamilisha ujenzi wa miundombinu na kuleta mitambo ya kisasa ambayo ni rafiki kwa mazinigira ili waendelee na uzalishaji.

Kwa upande wao wakazi wa eneo linalozunguka kiwanda wamepongeza maamuzi yaliyotelewa na Waziri kwa madai kuwa ni kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakiathirika na harufu kali, moshi, vumbi na kelele zinazotokana na shughuli katika kiwanda hicho.

Waziri Simbachawene amesema Serikali itaendelea kusimamia sheria na kanuni za mazingira ili kulinda mazingira na kuendelea kutatua kero za wananchi katika maeneno mbalimbali nchini kutokana na adha wanazokumbana nazo juu ya uchafu wa mazingira.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Ukraine yaamini ndege ilitunguliwa na kombora la Iran.

Read Next

Wafurahia daraja kukatika na kuomba lisikarabatiwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!