Ukraine yaamini ndege ilitunguliwa na kombora la Iran.

Viongozi mbalimbali wa Mataifa ya Magharibi wamesema Ushahidi unaashiria kuwa kombora la Iran lilitungua ndege ya abiria ya Ukrain iliyoanguka karibu na Tehran kimakosa na kutaka kufanyike uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi kilichosababisha ajali hiyo iliyoua watu 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo kupoteza maisha.

Ukraine awali ilisema kuwa inachunguza endapo ndege yake iliangushwa na kombora, jambo ambalo mamlaka za Iran zilikanusha vikali. Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.

Awali kwa mujibu wa Vyombo vya habari nchini Marekani maafisa wa serikali ya Marekani wanaamini ndege hiyo ilidunguliwa na kombora na kuiangusha karibu na Jiji la Tehran ambapo baadhi ya vyombo vya kijasusi vilinukuliwa vikidai kuwa picha za satelaiti zilionyesha mwanga wa makombora mawili ambao ulifuatiwa na mwanga wa mlipuko.

Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo hatua ambayo inatokana na mzozo uliopo baina ya Marekani na Iran hasa baada ya Rais Trump kuagiza Shambulio lililomuua Jenerali wa Iran Qasem Soleiman Januari 03.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Dkt. Shein azindua daraja la Kibonde Mzungu.

Read Next

Kiwanda chafungiwa kwa kukiuka kanuni na sheria za mazingira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram