Wahofia usalama wa afya kutokana na kutiririka majitaka.

Wakazi wa Mtaa wa Lindi katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam pamoja na maeneo yanayozunguka eneo hilo katika halmashauri hiyo wapo katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kutokana na kutapakaa na kutiririka kwa majitaka ambayo yameenea katika eneo hilo mithiri ya Maji ya Mvua.

Wakazi hao wanadai kuwa hali hiyo inawafanya kuishi kwa wasiwasi wa kulipuka magonjwa kutokana na Chemba kubwa ya Majitaka kutiririsha majitaka takriban mita 400 kuelekea katika Makazi ya watu hali ambayo imekuwa ikisababisha harufu kali wakati wote.

Aidha Maji hayo ambayo yanadaiwa kutiririka kwa zaidi ya Mwezi Mmoja na Nusu yamesababisha barabara hiyo kutopitika kutokana na kuharibika vibaya na kuwa mashimo pamoja na madimbwi ya maji yaliyotwama.

Wakizungumzia hali ya Ubovu wa barabara wamedai kuwa licha ya barabara hiyo kuwa muhimu katika kupunguza msongamano katika barabara ya uhuru lakini imekuwa ikisahaulika na kuzitaka mamlaka husika kuitupia macho.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Iran yaikaribisha kampuni ya Boeing kushiriki uchunguzi.

Read Next

Hospitali ya Mnyamani wamshukuru Rais Magufuli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!