Usimamizi fedha za Elimu waleta matokeo chanya.

Serikali imesema umakini katika kusimamia fedha zinazotolewa na wadau wa maendeleo katika mpango wa elimu bila ya malipo, umechochea ufaulu wa kiwango cha juu ikilinganishwa na kipindi cha miaka minne iliyopita ambapo kutokana na hilo itaendelea kusimamia rasilimali fedha kadiri zinavyopatikana kwa lengo la kuimarisha elimu nchini.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Lazaro Ndalichako, ameeleza kwenye hotuba ya kukabidhi magari 39 kwa Vyuo vya Elimu vya Serikali na vituo vya usimamizi na ufuatiliaji katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa taasisi ya Elimu Tanzania.

Prof. Ndalichako ameongeza kuwa udhibiti wa hali ya juu uliooneshwa na Serikali katika matumizi sahihi ya fedha hizo katika mradi ujulikanao kulingana na matokeo uliotekelezwa kwa pamoja na wadau wa maendeleo kama Benki ya Dunia, DFID, SIDA na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ndio umewezesha mafanikio yanayoonekana katika Sekta ya Elimu kukiwepo na ongozeko la wanafunzi katika shule za msingi na sekondari.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TAKUKURU yatakiwa kukamilisha uchunguzi mapema.

Read Next

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!