Serikali ya Ilala yaridhishwa na Ujenzi wa miradi.

Serikali ya Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam imeelezea kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kisutu, ambalo linatarajia kukamilika August mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ambaye amefanya ziara ya kukagua miradi mikubwa ya kijamii inayotekelezwa kwenye wilaya hiyo amemhimiza mkandarasi anayejenga soko hilo kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo kwa wakati ili kuwawezesha wafanyabiashara kuanza kulitumia.

Aidha amesema iwapo soko hilo linalojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 13.48 litakamilika linatarajiwa kuwa na wafanyabiashara mbalimbali, hatua ambayo itaiwezesha Serikali kupata mapato yake huku soko hilo likiwa limesogeza huduma kwa Jamii.

Naye Mkandarasi wa ujenzi wa soko hilo la Kisutu Taher Gulam Husein amesema hadi kufikia mwezi huo watakuwa wamekamilisha Ujenzi huo na soko kuanza kutumika.

Ujenzi wa jengo Hilo umemtumia zaidi ya Bilioni 13.48 na itaweza kuwahudumia wanachi mbalimbali.

Mradi mwingine aliotembelea Mkuu huyo wa wilaya ni Ujenzi wa Machinjio Vingunguti, ambako ametoa maagizo kwa mshauri wa ujenzi kufika katika mradi huo kwa ajili ya kutoa kwa baadhi ya maamuzi ya ya Ujenzi unaondelea katika Machinjio hayo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Read Next

Benki ya Dunia yaahidi kusaidia miradi ya maendeleo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!