Shambulio la Kigaidi lauwa Walimu watatu Kenya.

Raia watatu wameuawa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab kuvamia mji wa Garisa Kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Walimu watatu ambao si wa eneo hilo walipigwa risasi hadi kufa huku kituo cha polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.

Washambuliaji hao pia wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.

Maafisa wa polisi wanawafuatilia wahalifu hao huku ripoti za kiusalama zikionyoesha kwamba wavamizi hao waliweka vilipuzi chini ya ardhi katika barabara ya eneo hilo.

Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.

Wiki iliyopita, Uingereza ilitoa onyo kwa raia wake wanaotaka kusafiri kwenda kaunti ya Garissa na katika eneo la ndani ya kilomita 60 katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Hili ni shambulizi la 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi manne yalitokea Garissa, matatu Wajir, mawili Mandera na mawili mengine katika mji wa Lamu.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Watumishi wanaouza fomu za NIDA waonywa.

Read Next

Polisi na vikosi vya usalama vyawashambulia waandamanaji nchini Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!