Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Katika kipindi cha utawala wa Serikali ya awamu ya tano, mamlaka ya maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepata mafanikio makubwa ikiwemo ununuzi wa mitambo 9 yenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 9 ambayo imesaidia kupunguza siku za uchunguzi wa sampuli kutoka siku 21 hadi dakika 40 mpaka siku 2.

Hayo yamebainishwa Jijini Dsm na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko alipokuwa akizungumzia kampeni ya “Tunaboresha chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto” yenye lengo la kutembelea taasisi zote za wizara hiyo pamoja na hospitali za mikoa.

Dkt. Mafumiko amesema uwepo wa mitambo hio umeleta matokeo chanya hata kwenye upimaji wa vinasaba akitolea mfano utambuzi na uchunguzi wa miili iliyoharibika mfano ni ile ya ajali ya lori la mafuta lililolipuka mkoani Morogoro.

Aidha ametoa elimu kwa jamii ya Kitanzania kuhusiana na taratibu za kufanya uchunguzi wa vinasaba vya binadamu kwamba ni lazima kuwepo na maombi ya familia husika yatakayowasilishwa na kwa mkemia mkuu na wakili au afisa ustawi wa jamii ambaye ndie atakuwa mpokeaji wa majibu baada ya kufanyika kwa uchunguzi utakaowashirikisha wahusika wote.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Usimamizi fedha za Elimu waleta matokeo chanya.

Read Next

Serikali ya Ilala yaridhishwa na Ujenzi wa miradi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!