Hospitali ya Mnyamani wamshukuru Rais Magufuli.

Uongozi wa kilichokuwa Kituo cha Afya cha Buguruni kwa Mnyamani ambapo hivi sasa Kituo hicho kimepanda hadhi na kuwa Hospitali ya Mnyamani umemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za Ujenzi wa Majengo ya Mama na Mtoto lakini pia kituo hicho kupatiwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji.

Shukrani hizo zimetolewa na Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt. Stefano Sambuli wakati Uongozi wa Manispaa ya Ilala ukiongozwa na Mstahiki Meya wa Ilala walipokwenda kukagua ujenzi wa majengo mapya yanayojengwa katika eneo la Hospitali hiyo kwa ajili ya huduma ya Mama na Mtoto.

Dkt. Stephano amesema katika hospitali hiyo kumekuwa na ongezeko la wananchi wanaopatiwa huduma kila siku ambapo kwa wastani akinamama 350 hadi 500 hupatiwa huduma kila siku na kubainisha kuwa kukamilika kwa majengo hayo kutapunguza Msongamano wa wananchi.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Omar Kumbilamoto Pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Elizabeth Thomas wamesema Hospitali hiyo hivi sasa imekuwa tegemeo kubwa kwa wananchi kutoka maeneo mbali mbali kutokana na kuboreshwa katika eneo la utoaji huduma ambapo hivi sasa huduma za upasuaji kwa wajawazito zimekuwa zikitolewa bila malipo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wahofia usalama wa afya kutokana na kutiririka majitaka.

Read Next

Watumishi wanaouza fomu za NIDA waonywa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!