Watumishi wanaouza fomu za NIDA waonywa.

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Bw. Filberto Sanga amewataka watendaji wa kata, vijiji na wataalam wengine kujieupusha na tabia ya kuchukua fedha kwa wananchi ili wawapatie fomu za kitambulisho cha taifa NIDA na yeyote atakayekutwa akifanya hivyo Serikali haitosita kuchukua hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliolenga kusikiliza kero za wananchi, Bw. Sanga amesema tabia ya wasimamizi wa NIDA kwa ngazi ya kata na vijijji kuwauzia fomu wananchi hakikubaliki kutokana na huduma hiyo kutolewa bure hivyo yeyote atakayebainika serikali haitosita kuchukua hatua kali za kinidhamu.

Katika hatua nyingine Bw. Sanga amewataka wananchi wa Mwandege kujitokeza kushiriki katika zoezi la urasimishaji ardhi pindi zoezi hilo litakapoanza huku akiwataka wale wote watakaotakiwa kupisha ujenzi wa miradi ya maendeleo kuwa na moyo wa uzalendo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Hospitali ya Mnyamani wamshukuru Rais Magufuli.

Read Next

Shambulio la Kigaidi lauwa Walimu watatu Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!