Polisi na vikosi vya usalama vyawashambulia waandamanaji nchini Iran.

Polisi nchini Iran pamoja na vikosi vya usalama nchini humo vimefyatua risasi na mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliojitokeza kupinga hatua ya mwanzo iliyochukuliwa na jamhuri hiyo ya Kiislamu kukanusha kuhusika na udunguaji wa ndege ya Ukraine.

Hakuna ripoti iliyotolewa mara moja na televisheni ya taifa ya Iran kuhusu tukio hilo lililotokea karibu na uwanja wa uhuru mjini Tehran jana Jumapili usiku.

Hata hivyo mashirika ya haki za binadamu ya kimataifa tayari yamekwishaitaka Iran kuwaruhusu watu kuandamana kwa amani kama inavyotajwa kwenye katiba.

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha haki za binadamu chenye makao yake NewYork Marekani, Hadi Ghaemi amesema Wairani hawapaswi kuhatarisha maisha yao kuendesha haki yao ya kikatiba ya kukusanyika.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Shambulio la Kigaidi lauwa Walimu watatu Kenya.

Read Next

TAKUKURU yatakiwa kukamilisha uchunguzi mapema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!