TAKUKURU yatakiwa kukamilisha uchunguzi mapema.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ukamilishe mapema uchunguzi dhidi ya madudu yaliyoibuliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 na wizi uliofanywa na viongozi wa AMCOS kwa wakulima wa Ufuta na Korosho ikiwemo Wilaya ya Ruangwa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Ruangwa lililogharimu zaidi ya Tsh. milioni 142 ambapo ameitaka taasisi hiyo kuwa imara na kutembea kifua mbele katika mapambano hayo.

Waziri Mkuu amesema pamoja na TAKUKURU kuendelea na utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku pia ameuagiza uongozi wa taasisi hiyo ukamilishe mapema utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa kwao kwa nyakati tofauti.

Amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imekuwa ikijipambanua na vita dhidi ya rushwa na ufisadi ambapo itaendelea kudhibiti mianya yote ya rushwa katika utendaji mzima wa Serikali.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema hadi sasa wamefanikiwa kuokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 1.042 zilizokuwa mali ya wakulima wa ufuta ambao walidhulumiwa fedha hizo na Viongozi wa Vyama vya AMCOS na kwamba kazi bado inaendelea, lakini pia akiweka wazi namna taasisi hiyo ilivyojipanga kudhibiti rushwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Polisi na vikosi vya usalama vyawashambulia waandamanaji nchini Iran.

Read Next

Usimamizi fedha za Elimu waleta matokeo chanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!