Benki ya Dunia yaahidi kusaidia miradi ya maendeleo.

Benki ya dunia imeahidi kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo nchini ikiwemo maendeleo ya miundombinu, lakini zaidi kusaidia maendeleo ya shughuli za kijamii hususani afya na elimu.

Aidha kutokana maendeleo pamoja na ufanisi unaoonekana wa miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Benki ya Dunia ni kielelezo muafaka cha dhana ya kuboresha maisha ya watu na uthibitisho kuwa Benki ya Dunia inaridhishwa na uwekezaji wake kwenye miradi hiyo.

Hayo yamesemwa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini anayemaliza muda wake, Bella Bird wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoandaliwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, ambapo amesema ni azma ya taasisi yake kuendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania kwa lengo la kuboresha maisha ya watu hususani kuondoa umaskini.

Kuhusu TASAF, Bi. Bird ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa nchi pekee barani Afrika yenye taasisi imara kwa ajili ya maendeleo ya jamii, huku akisema mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na TASAF ni miongoni mwa miradi inayorandama na kazi za Benki ya Dunia.

Akitoa shukrani na pongezi kwa Mkurugenzi huyo ambaye sasa anakwenda kuwa Mshauri wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia kuhusu masuala ya Afrika, Mkurugenzi Mkuu wa TASAF Dkt. Ladislaus Mwamanga amesema TASAF na Benki ya Dunia zimefanikiwa kuzifikia kaya masikini na ambazo kwa sasa zimepata ahueni ya maisha baada ya kusogezewa huduma za kijamii.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali ya Ilala yaridhishwa na Ujenzi wa miradi.

Read Next

Wauza matunda Kariakoo wakiuka kanuni za Afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!