Iran yawakamata waliodungua ndege ya Ukraine.

Iran imetangaza leo kwamba watu kadhaa wamekamatwa kuhusiana na kombora lililorushwa kimakosa na kuiangusha ndege ya Ukraine karibu na uwanja wa ndege wa Tehran na kuwauwa watu wote 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Tangazo hilo limekuja muda mfupi baada ya Rais Hassan Rouhani kutaka iundwe mahakama maalum kushughulikia mkasa huo. Msemaji wa idara ya mahakama, Gholamhossein Esmaili, aliyetoa tangazo hilo, hakubainisha idadi ya watu waliotiwa mbaroni.

Tayari Marekani imejiondoa katika makubaliano hayo na Iran imesema itaacha kuheshimu ukomo wa kurutubisha madini ya uranium uliowekwa katika makubaliano hayo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

TRA wahimizwa kuongeza bidii ya kukusanya mapato.

Read Next

Jeshi la Sudan lakabiliana na uasi nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!