Wauza matunda Kariakoo wakiuka kanuni za Afya.

Kaimu Afisa Afya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam amewataka wafanyabiashara wa vyakula na Matunda yaliyomenywa na kuuzwa katika maeneo mbali mbali ya Kariakoo kuzingatia Kanuni za Afya na Usafi wa mazingira katika kuendesha biashara hiyo ili kulinda afya za walaji pamoja na kuzuia Uwezekano wa kuzuka milipuko ya magonjwa.

Akizungumza na Chanel ten wakati alipofanya ukaguzi katika Maeneo ya Kariakoo yanayouzwa vyakula na Matunda yaliyomenywa akifuatana na Afisa Mazingira wa Manispaa hiyo Cosmas Mwaitete ameshuhudia biashara ya matunda yaliyomenywa ikifanyika bila kuzingatia kanuni za Usafi hali inayoweza kusababisha madhara kwa walaji.

M/kiti wa wafanyabiashara wa Matunda katika soko hilo la Kariakoo Haruna Maliki amekiri kuwepo na mapungufu katika biashara zao kwa kuendesha biashara bila kuzingatia kanuni za Afya na kuahidi kulifanyia kazi huku baadhi ya wananchi wakipongeza jitihada za kuwapa elimu wafanyabiashara ili waendeshe biashara zao katika mazingira ya usafi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Benki ya Dunia yaahidi kusaidia miradi ya maendeleo.

Read Next

TRA wahimizwa kuongeza bidii ya kukusanya mapato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!