TRA wahimizwa kuongeza bidii ya kukusanya mapato.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amewahimiza watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, na kwa kuzingata misingi wa Sheria za kodi ili kuhakikisha kuwa TRA inaendelea kuvunja rekodi ya makusanyo ya mapato kama ilivyokuwa katika miezi ya Septemba na Desemba, 2019.

Pia, amewapongeza watumishi wote wa Mamlaka hiyo kwa kujituma na kuiwezesha Serikali kukusanya mapato ya kiasi cha Tsh. trilioni 9.341 sawa na ufanisi wa asilimia 47.67 ya lengo la kukusanya Tsh. trilioni 19.595 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka 2019/2020 yaani kuanzia Julai hadi Desemba 2019.

Alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi wa nusu mwaka 2019/20 wa Mamlaka hiyo uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Edwin Mhede, alieleza kwamba mkutano huo wa mapitio na tathmini ya nusu mwaka ulilenga kufanya maboresho katika utendaji kazi ili kuhakikisha kuwa malengo waliyopangiwa na Serikali yanafikiwa.

Mkutano wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi wa nusu mwaka 2019/20 wa TRA ulihudhuriwa na jumla ya washiriki 361 ukihusisha Menejimenti nzima ya Mamlaka, Mameneja wote wa Mikoa na Wilaya kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wawakilishi kutoka baadhi ya Asasi za Serikali kama vile Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wauza matunda Kariakoo wakiuka kanuni za Afya.

Read Next

Iran yawakamata waliodungua ndege ya Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!