Raia wa Iran watakiwa kuingia mitaani zaidi kwa maandamano.

Maandishi katika mitandao ya kijamii nchini Iran yamewahimiza raia wa nchi hiyo kuingia mitaani kwa siku ya tano mfululizo leo, baada ya hasira ya umma kuzuka kufuatia hatua ya kukiri kwa maafisa wa serikali kuwa ndege ya abiria ya Ukraine iliangushwa kimakosa wiki iliyopita.

Waandamanaji wakiongozwa na wanafunzi wamefanya maandamano ya kila siku mjini Tehran pamoja na miji mingine tangu Jumamosi, wakati maafisa wakikiri kuhusu kuangushwa kwa ndege hiyo ya abiria ya Ukraine wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu wote 176 waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya siku kadhaa za kukana.

Rais wa Iran ameuita mkasa huo wa kuanguka ndege kuwa ni makosa ambayo hayawezi kusahaulika na jeshi limeomba radhi huku mahakama ikisema imewakamata baadhi ya wale inaowashutumu kuwajibika na ajali hiyo katika juhudi za kupunguza hasira ya wananchi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Jeshi la Sudan lakabiliana na uasi nchini humo.

Read Next

Tanzania na Sweden zasaini makubaliano ya msaada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!