Mkazi wa Kibondo ataka kujiua baada ya kumuua mkewe.

Mkazi mmoja anayeishi wilaya Kibondo Mkoani Kigoma Albert Rugai miaka 65 amejaribu kujiua kwa kunywa sumu baada ya kumuua mke wake Ester Kondo miaka 45 kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi pamoja na kugombania mali ambazo walizonazo.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea mwanzoni mwa juma hili nyumbani kwa Albert Rugai baada ya kutokea ubishi kati yake na mke wake unaohusisha kugombania nyumba waliyojenga pamoja ambapo mke alitaka hati ya nyumba iandikwe jina lake jambo lililosababisha kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani mpaka kufa.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kibondo Dkt. Mathias Bwashi amethibitisha kupokea mwili wa marehemu pamoja na mume wa marehemu aliyejaribu kujiua kwa kunywa sumu ambaye tayari amepokea matibabu.

Jeshi la Polisi limethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea huku wakiwa wamemshikilia mtuhumiwa Albert Rugai anayetuhumiwa kumuua mke wake.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wadau wajadili changamoto za usafirishaji majini.

Read Next

Mabenki yanayotoa mikopo ya nyumba yapongezwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!