Mabenki yanayotoa mikopo ya nyumba yapongezwa.

Serikali imesema hatua ya Taasisi za fedha kuanza kutoa mikopo ya muda mrefu ya ujenzi wa nyumba utawawezesha watanzania wengi kupata uwezo wa kujenga nyumba bora, pamoja na kutumia nyumba hizo kujiinua kiuchumi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema wizara yake hivi sasa imeelekeza nguvu zaidi katika upimaji na urasimisha makazi katika maeneo mbalimbali nchini ili kila mwananchi anaemiliki ardhi aweze kuwa na hati ambayo inatambulika kisheria, hivyo hatua ya mabenki kuanza kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba ya muda mrefu kati ya miaka kumi na mitano hadi ishirini, ni kuunga mkono jitihada hizo za serikali ambazo lengo lake kuu ni kuwawezesha watanzania kutumia ardhi yao kuwainua kiuchumi.

Kwa upande wa Benki ya NMB ambao ndio wamezindua mikopo hiyo ijulikanayo kwa jina la Nyanyua Mjengo, mikopo ambayo Mtanzanai yeyote mwenye kiwanja chenye hati ya serikali anastahili kupata wamesema mikopo hiyo itakuwa na riba ya asilimia kumi na saba, huku mkopo wa juu ukiwa ni Shilingi million mia mbili.

Takwimu zinaonyesha kuwa tanzania inahitaji nyumba zaidi ya laki mbili kwa mwaka, huku asilimia 75 ya nyumba bora zilizopo mijini hazina hati hivyo haziwezi kutumika kwenye taasisi za kifedha kama dhamana pale wahusika wakihitaji kukopa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mkazi wa Kibondo ataka kujiua baada ya kumuua mkewe.

Read Next

Bunge la Marekani na azimio kumng’oa Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!