Jeshi la Sudan lakabiliana na uasi nchini humo.

Jeshi la Sudan linayashikilia makao makuu ya kikosi cha usalama wa taifa cha nchi hiyo ambacho awali kilikuwa kitiifu kwa rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir ambapo Jeshi hilo linatarajia kukivunja Kitengo hicho na kuunda kipya kutokana na madai ya uasi.

Serikali inaadai kuwa uasi huo umechochewa na malipo ya mafao, lakini pia kuna mashaka juu ya tukio hilo kulenga kuchelewesha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Kiongozi mwandamizi wa baraza huru linaloongoza Sudan kwa sasa, Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, amemtuhumu mkuu wa zamani wa usalama wa taifa Salah Gosh kuwa yupo nyuma ya uasi huo Japo Dagalo anasema hachukulii jambo hilo kama jaribio la mapinduzi, lakini amesema jambo hilo halivumiliki.

Kumekuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa baadhi ya viongozi waliokuwa na ushawishi wakati wa Bashir kujaribu kutatiza mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo kwa hivi sasa.

Bashir ambaye alikaa madarakani kwa mkono wa chuma kwa miaka 30 alipinduliwa mwezi Aprili mwaka jana baada ya kuchachamaa kwa maandamano ya umma ya kumtaka aondoke madarakani

Askari kutoka kitengo cha usalama wa taifa walipakia mtandaoni picha za video zikionesha wenzao wakifyatua risasi hewani usiku kama alama ya uasi na kuonesha nguvu zao.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Iran yawakamata waliodungua ndege ya Ukraine.

Read Next

Raia wa Iran watakiwa kuingia mitaani zaidi kwa maandamano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!