Tanzania na Sweden zasaini makubaliano ya msaada.

Serikali ya Tanzania imetiliana saini mikataba miwili ya msaada na serikali ya Sweden kwa kupatiwa fedha kiasi cha dola milioni 90 sawa na shilingi Bilioni 240.95 kutoka mfuko wa ushirikiano wa Elimu Duniani GPE.

Akizungumzia msaada huo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wizara ya fedha na mipango Dotto James ameitaja miradi hiyo kuwa ni shilingi bilioni 88.55 zitagharamia mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu (ESDP) 2016/17 – 2021/2022 katika sekta tatu ndogo ikiwemo elimu ya msingi, elimu jumuishi, watu wazima na iliyo nje ya mfumo rasmi.

Bilioni 116.40 zitaongeza mchango wa Serikali ya Sweden katika Program ya Elimu kwa matokeo (EPforR) lengo likiwa ni kuwezesha mpango wa maendeleo ya sekta ya elimu 2016/17 – 2021/22 hususan kuwezesha ubora na usawa katika matokeo ya elimu ya msingi na sekondari.

Mkataba uliosainiwa leo unatokana na mfuko ambao unachangiwa na washirika wa maendeleo wengine wakiwemo UNICEF, UNESCO, Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya, Australia, Canada, Denmark, Ufaransa, Korea, Uholanzi, Norway, Hispania, Uswis, Marekani na Uingereza.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Raia wa Iran watakiwa kuingia mitaani zaidi kwa maandamano.

Read Next

Wadau wajadili changamoto za usafirishaji majini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!