Wadau wajadili changamoto za usafirishaji majini.

Wadau wa usafirishaji Duniani kwa njia ya bahari na majini wamekutana jijini dar es salaam kujadili changamoto za usafirishaji na kuzitafutia ufumbuzi, Tanzania ikibahatika kuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya pili katika mzunguko wa mikutano 24.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema Dunia imeiona Tanzania kuwa inafanya vizuri katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji ikiwemo maboresho makubwa katika bandari zote huku bandari ya Dar es salaam ikiongezewa kina cha bahari pamoja na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa mizigo.

Mhandisi Kamwelwe amesema wadau wa usafirishaji wanafahamu kuwa Tanzania kuna soko na kwamba serikali iko kwenye mchakato wa kutafuta mkandarasi wa kuongeza mlango wa bahari ili kuruhusu meli zenye kubwa na uzito mkubwa kuweza kuingia Tanzania kupitia bandari na kuondoa ucheleweshwaji wa mizigo.

Mkurugenzi mkuu mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema asilimia 80 ya biashara inatumia usafirishaji wa majini duniani, hivyo kuchaguliwa kwa Tanzania kuwa wenyeji wa mkutano huu mara mbili katika mikutano 24 inayoshirikisha nchi zote Duniani ni matokeo ya wadau kutambua kuwa Tanzania ina uwezo wa kuendesha biashara hiyo huku akibainisha kuwa Tanzania ina kilomita za maji zaidi ya 1440.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Tanzania na Sweden zasaini makubaliano ya msaada.

Read Next

Mkazi wa Kibondo ataka kujiua baada ya kumuua mkewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!