Bunge la Marekani na azimio kumng’oa Trump.

Baraza la Wawakilishi nchini Marekani limepitisha azimio la kuwasilisha mashtaka dhidi ya Rais Donald Trump katika Bunge la Senate kitendo ambacho kinaashiria kuanza kwa kesi inayoweza kumuondoa madarakani Rais huyo.

Wabunge 228 walipitisha azimio hilo huku 193 wakipinga hatua ambayo inamaanisha kuwa Bunge la Senate ambalo linadhibitiwa na Maseneta wa Chama cha Rais Trump cha Republican watapata nafasi ya kusikiliza madai ya Trump na kuyapigia kura.

Hatua hiyo imekuja katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja, tangu Wabunge wa Baraza hilo kumkuta na hatia Rais Trump ya matumizi mabaya ya madaraka na kuzuia juhudi za Bunge kuchunguza vitendo vyake.

Mwaka uliopita, Bunge la Wawakilishi ambalo linaongozwa na chama cha Democratic, walipigia kura ya kumwondoa madarakani Rais Trump kwa kutumia vibaya madaraka yake lakini pia, kudharau bunge hilo.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mabenki yanayotoa mikopo ya nyumba yapongezwa.

Read Next

Wanaume zaidi ya 600 waripotiwa kupigwa na wenza wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!