China na Marekani zatia saini hatua ya kwanza ya mkataba wa kumaliza vita vya kibiashara.

China itaongeza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka Marekani zenye thamani ya dola Bilioni 200 mnamo kipindi cha miaka miwili ikiwa ni sehemu ya mkataba uliotiwa saini baina ya Rais Donald Trump na makamu wa Rais wa China Wang Qishan.

Kwa upande wake Marekani itaondoa ushuru ilioweka kwenye baadhi ya bidhaa dhidi ya China. Hata hivyo mkataba huo ni hatua ya kwanza katika juhudi za kuvimaliza vita vya kibiashara baina ya nchi mbili hizo zinazoongoza katika nguvu za kiuchumi duniani.

Ustawi wa uchumi wa dunia uliathirika kutokana na vita hivyo vya kibiashara ambavyo hadi sasa vimechukua muda wa mwaka mmoja na nusu.

Hisa zilipanda kwenye masoko muhimu ya dunia baada ya mkataba huo kutiwa saini mjini Washington hapo jana. Licha ya kusifu mkataba huo kuwa ni ushindi kwa uchumi wa Marekani, Rais Trump amekiri kwamba bado pana haja ya kuzungumzia masuala mengine ambayo hayajatatuliwa.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Wanaume zaidi ya 600 waripotiwa kupigwa na wenza wao.

Read Next

Spika Ndugai aongoza mazishi ya Mbunge wa Newala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!